Kwa huu muda ambamo ulimwengu wapambana na janga la COVID-19, waongozi wa kata fulani katika jiji la Butembo, hawaheshimu tena mikakati ya kunawa mikono. Wageni waingia katika ofisi zao bila kunawa mikono na bila kutishwa ajapo kua walikua wamezoeya kuwosha mikona wakati Ebola ilikua nafanya maafa katika muji wa Butembo.

Wakati kipindupindu ya Ebola ilizuka jijini Butembo, wafazili wa gavumenti ya congo wanao tumika na timu ya kupiganisha Ebola, walipana vyombo vya kunawa mikono kwa kata zote za Butembo. Kila mgeni, mbele aingiye katika ofisi, alikua naosha mikono bila tatizo. Ajapokua janga ya Ebola na Corona bado kutangazwa kumalizika, katika kata fulani hakuna tena kunawa mikono mbele kuingia katika ofisi. Vyombo ambavyo wafazili walipana, vimebebwa na viongozi. Tulipenda kuwasiliana na viongozi wa kata fulani za Butembo, lakushangaza, walitukimbia. Wachache walio wasiliana nasi, walikiri kwamba vyombo vya kuosha mikono vimechukuliwa nyumbani mwao kwa matumizi binafsi. Waongozi makamu wachongea waongozi wasimamizi wa kata kuchukua vyombo, mukiwemo Tanki na mbegeti mbalimbali. Mukiingia nyumbani mwao, mutakuta hivyo vyombo, waliongeza kusema hao waongozi naibu wakinungunika. Kupita katika mtaa wa Bulengera, kutokea Kimemi na Mususa, kumalizia Vulamba, hali ya kukosewa vyombo vya kuosha mikono ni sawa. Katika kata chache ambamo tulikuta vyombo vya kunawa mikono, tulikuta hamuna maji, na kwenye kunakua maji kakuna sabuni. Sasa, ni nani ndiye anahukika kutia maji katika tanki na mbegeti za kuosha mikono ? swali hilo halikupata jibu kwa waongozi wa kati. Inaonekana kwamba wanajichongea. Tulipenda kufahamu zaidi kuhusu hilo jambo, tulimuita bwana Jean De Dieu SANGALA, mwongozi wa kata Kyaghala, yeye ni msimamizi wa waongozi wote katika jiji la Butembo. Alihakikisha kujibu kwa maswali zetu siku zijazo.

Mfahamu kwamba kunawa mikono ni mojo ya kanuni za kupiganisha Ebola na Coronavirus.